Wizara ya Madini kuimarisha Utendaji GST

WIZARA ya Madini imejipanga kuimarisha utendaji kazi wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ili kuiwezesha kufanya tafiti za kina na kuongeza uwigo wa upatikanaji wa taarifa sahihi za maeneo ya uchimbaji.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo ameweka wazi mipango hiyo wakati akizungumuza na wachimbaji wadogo katika warsha iliyofanyika viwanja vya Maonyesho ya Teknolojia ya Madini mjini Geita.

Mbibo amesema “tutaendelea kuiimarisha taasisi hii ili iwe na uwezo mkubwa na kutupatia taarifa ambazo ni za kina kwa maeneo ambayo yana madini na kuachana na ile ya watu kwenda kubahatisha bahatisha tu na kupelekea mitaji yao kukatika.

“Hili ni jambo ambalo tumedhamiria ndani ya wizara yetu, kusimamia nsa kuhakikisha kwamba taasisi hii inakuwa bora zaidi, na hapa Geita tayari tumeshaanzisha hiyo maabara ya madini na inaendelea kufanya kazi.

Ameitaja ofisi ya GST mkoa wa Geita kuwa miongoni mwa ofisi zitakazoboreshwa kwa kuongezewa wafanyakazi na vitendea kazi ili kuwafanya waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa kuwahudumia wachimbaji wadogo.

Kwa upande wa Ofisa wa GST Mkoa wa Geita, John Kalemanzi amewashauri wachimbaji wadogo kuachana na njia za kutumia rangi ya udongo kung’amua kiwango cha madini badala yake wafike maabara ya GST kupata taarifa sahihi za kijiolojia.

Amekiri iwapo watawezeshwa itawasaidia kuwafikia wachimbaji wadogo wengi zaidi ingawa ndani ya mwaka mmoja hadi sasa wamefanikiwa kuwafikia takribani wachimbaji wadogo 350 mkoani Geita ndani na kuwapatia elimu ya jiolojia.

Amesema pia kusogezwa kwa huduma ya maabara ya madini mkoani Geita imeongeza idadi ya sampuli za udongo wa madini wanazopokelewa kwa wiki kutoka sampuli 7 hadi 10 hadi kufikia sampuli 30 ndani ya wiki moja katika ofisi za GST Geita.

Nae, Mwenyekiti wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo mkoani Geita (GEREMA), Christopher Kadeo alimeiopongeza GST chini ya Wizara ya Madini kwa kusogeza huduma mkoani Geita na sasa wachimbaji wengi wadogo wamenufaika

Habari Zifananazo

Back to top button