DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde amesema wizara hiyo imejipanga kutumia njia za kisasa za kupata taarifa za kijiolojia kupitia mpango wa “Vision 2030, Madini ni maisha na Utajiri”, ili kuhakikisha sekta ya madini inalinuafaisha taifa, hivyo kuboresha maisha ya Watanzania.
Amesema hatua hiyo inatokana na ukweli kwamba ni asilimia 16 ya maeneo ya Tanzania yaliyofanyiwa tafiti za kisasa kubaini taarifa za kijiolojia za uwepo wa madini
Kiongozi huyo ameyasema hayo leo Oktoba 25, 2023 katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).
“Tunaamini kuwa utekelezaji wa dira ya 2030 itakuwa chachu katika upatikanaji wa madini nchini,” amesema Mavunde.
Mkutano huo ni wa siku mbili, hadi Oktoba 26, 2023 na unahudhuriwa na viongozi, washiriki na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Comments are closed.