Wizara ya Maji kufufua visima 197 Dar

SERIKALI kupitia Wizara ya maji leo imetoa mitambo mipya ya kufufua visima 197 na kujenga mabwawa ili kukabiliana na uhaba wa maji katika jiji la Dar Es Salaam na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani .

Akizungumza wakati wa kukagua mitambo hiyo ya kuchimba visima na kujenga mabawawa, Waziri wa Maji ,Jumaa Awesso amesema mitambo hiyo itatolewa katika kila Wilaya nchi nzima ili kuvuna na kutunza maji kwa ajili ya matumizi ya kilimo,ufugaji na matumizi ya watu.

“Naagiza visima 197 vifufuliwe  na kuingizwa katika mfumo  na wana Dar es Salaam waendelee kupata maji safi na salama , mnafanya kazi usiku na mchana hizo changamoto wakati zingine ziwe funzo kwetu,”ameagiza Aweso.

Amesema hapa nchini kuna  maji chini ya ardhi na juu ya ardhi mita za ujazo bilioni 126 ambapo  bilioni 105 ya maji yako juu ya ardhi na bilioni 21 ni maji yaliyokuwa chi ni ya ardhi.

Amesema jukumu la kulinda vyanzo vya maji ni wananchi wote  kwani wameshuhudia mwaka jana na huu uhaba wa maji na  haya kuwa mafunzo kwa kujua kuwa  mazingira ukiyalinda yatakulinda, usipoyalinda yatakuadhibu.

Amesema awali DAWASA ilikuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 520 lakini sasa wanaweza  kuzalisha maji lita milioni 300 hivyo wanakiri upungufu  na jana wamepata lita milioni 70 Kigamboni ambazo zitatumika kwa wananchi.

Habari Zifananazo

Back to top button