NAIBU Waziri wa Ardhi, Geofrey Pinda amesema ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa, wizara itamaliza vikwazo vinavyochelewesha ujenzi wa stendi ya kisasa eneo la Bondeni City mkoani Arusha.
Pia ametoa mbili kwa makamishna na maofisa ardhi nchi mzima kutoa hati za ardhi kwa wananchi na kuacha tabia ya ucheleweshwaji utoaji hati hizo, ili kuondoa malalamiko yanayotoa taswira mbaya katika wizara hiyo.
Amehoji kwa nini Arusha ikose stendi ya kisasa kwa sababu ya wivu tu wa baadhi ya watu na kwamba kama kuna maslahi ya mtu ijulikane.
Amesema wizara imelibeba jambo la stendi hiyo haraka, kwani wananachi wa Arusha wanahitaji stendi.
“Siasa za nini katika mradi huu wa Bondeni City, Benki ya Dunia imeshawekeza fedha sasa anatokea mtu mmoja ana maslahi gani, lazima stendi ijengwe na ndani ya mwezi huu watu waBenki ya Dunia wapate kibali, nimeuliza Jiji, Ofisi ya Mkoa wanasema hakuna tatizo sasa kwa nini mradi wa stendi usiendelee?”Amehoji.