Wizara yaanika vipaumbele maendeleo ya jamii

DODOMA; WAZIRI wa aendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima amesema mwaka wa Fedha 2024/25 , wizara hiyo kupitia idara na taasisi zilizopo chini yake imepanga kutekeleza vipaumbele sita,  ili kuboresha utoaji  huduma za maendeleo na ustawi wa jamii.

Waziri Gwajima amesema hayo wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025, ambapo amesema vipaumbele hivyo ni pamoja kukuza ari ya jamii kushiriki katika kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo iliyoibuliwa ngazi ya msingi.

“Kuratibu afua za kukuza usawa wa kijinsia na kutokomeza vitendo vya ukatili, uwezeshaji wanawake kiuchumi, upatikanaji wa haki, ulinzi na malezi chanya ya watoto,” amesema Waziri Gwajima na kuongeza kuwa wizara itafanya uratibu na kuimarisha utoaji wa huduma za msingi za ustawi wa jamii

Advertisement

Nyingine ni kutambua, kuratibu na kuendeleza makundi maalum wakiwemo wafanyabiashara ndogondogo, kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunzia katika taasisi na vyuo vya ustawi na maendeleo ya Jamii; na kuimarisha ushiriki na mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika maendeleo ya Taifa.