Wizara yahadharisha homa ya ini

WIZARA ya Afya imehadharisha wananchi na kuwataka wachukue hatua katika kukabiliana na ugonjwa wa homa ya ini ambao una madhara makubwa.

Tahadhari hiyo ambayo iimeainishwa  ni pamoja na kupata chanjo dhidi ya ugonjwa huo unaosababishwa na virusi ambavyo huambukizwa kwa njia mbalimbali.

Takwimu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) zinaonesha kuwa maambukizi ya Homa ya Ini aina ya B miongoni mwa wachangiaji damu kwa miaka mitatu kwa ni aslimia 4.4 mwaka 2018, asilimia 5.9 mwaka 2019, mwaka 2020 asilimia 6.1 na asilimia 5.3 mwaka 2021.

Naibu Waziri wa Afya Dk Godwin Mollel leo Julai 28,2023 amesema kwa sasa chanjo hiyo inapatikana katika Hospitali za Rufaa za mikoa, Hospitali za Rufaa za Kanda na katika hospitali zingine.

Siku ya Homa ya Ini Duniani huadhimishwa Julai 28, ikiwa na lengo la kutoa elimu na hamasa kuhusu ugonjwa huo.

 

Habari Zifananazo

Back to top button