KOCHA wa Barcelona, Xavi Hernandez amesema kiungo Sergio Busquets anayehusishwa kuondoka klabuni hapo Januari ataendelea kusalia mpaka mwisho wa mkataba wake.
“Busquets ataendelea kuwa nasi hadi mwisho wa mkataba wake mwezi Juni. Kisha tutaona, itakuwa ni uamuzi wake, mambo yakienda vizuri tutajaribu kumshawishi aendelee kusalia.” amesema Xavi
Xavi amesema kwa sasa hafikirii kuongeza mchezaji “Nadhani dirisha hili la usajili kwetu litakuwa kimya. Nina furaha sana na kikosi cha sasa.” Amesema Xavi.
Katika msimamo wa La Liga timu hiyo inaongoza ikiwa za pointi 37, nyuma ya Real Madrid wenye pointi 35, Atletico wanafuata wakiwa na 27