Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Burkina Faso, Yacouba Songne leo ameandika ujumbe wa kuwaaga wanajangwani baada ya kukosa nafasi kupenya katika dirisha dogo la usajili.
Kupitia Instagram Yacouba ameandika; “Ulikuwa wakati mzuri tangu tulipokuwa pamoja mpaka sasa asanteni kwa upendo wenu kwangu na ushirikiano wenu kwanzia kwa wachezaji hadi uongozi wote wa yanga na mashabiki daima nitawakumbuka hadi wakati mwingine wananchi asante sana na kwaherini nawapenda.
”
Agoust 11, 2020 Yanga ilitangaza kumsajili mchezaji huyo, kabla ya kutua Jangwani aliwahi pia kukipiga Asante Kotoko ya Ghana.
Yanga ipo kwenye harakati za kuimarisha kikosi chake, huku ikiwa imebaki siku moja dirisha la usajili kufungwa, tayari imenasa saini za baadhi ya wachezaji akiwemo, Kennedy Musonda, Mudathir Yahya.
pamoja na kumuongezea mkataba Khalid Aucho.