Yanga bado wana faida

AINA tatu ya matokeo watakayopata Yanga SC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Africa dhidi ya Club Africain yatawapa faida na dalili nzuri za kutinga katika hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Yanga itashuka katika Dimba la Hammedi Agrebi Olympic nchini Tunisia, kuvaana na waarabu hao, katika mchezo wa raundi ya pili utakaopigwa Saa mbili usiku wa leo kwa saa za Afrika Mashariki.
Matokeo ambayo Yanga wanahitaji ni sare yoyote ya mabao na ushindi wowote, matokeo haya yatawavusha kwenda hatua ya makundi, sare ya bila kufungana ambayo itawapeleka katika mikwaju ya  penalty ambapo yoyote anaweza kupenya.
Mchezo huo unakuwa tofauti na ule wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al- Hilal kwa maana ya kwamba makosa ambayo Yanga waliyafanya ni kuruhusu bao ambalo liliwapa faida timu hiyo, hivyo hata kama mechi ingeisha 0-0 Yanga alikuwa anatoka.
Kitendo cha kutoa sare katika mchezo dhidi ya Club Africain bado kinawapa faida Yanga kwa maana wanatakiwa kuhakikisha ndani ya dakika 90 hawapati bao lolote kwa kufanya hivyo Yanga huenda ikafuzu.

Habari Zifananazo

Back to top button