Yanga Bingwa 2022/23

YANGA ndiye bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2022/23, ikiwa ni mara ya pili mfululuzo baada ya kutwaa taji hilo msimu wa mwaka 2021/2022.
Hatua ya Yanga kuibuka bingwa inatokana na ushindi wa mabao 4-2 iliyoupata katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji uliomalizika muda mfupi Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yameifanya Yanga kufikisha pointi 74, ambazo ambazo haziwezi kufikiwa na washindani wao wa karibu Simba wanaoweza kufikisha pointi 73, kama wakishinda michezo yao miwili iliyobaki, huku Yanga hata kama ikipoteza michezo yake miwili iliyobaki hakuna kitakachoharibika.

Katika mchezo huo, Yanga ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Kennedy Musonda dakika ya 39 na mchezo kuisha kipindi cha kwanza Yanga ikiwa mbele.

Mchezaji Collins Opare aliisawazishia Dodoma dakika ya 59 na ubao kusomeka 1-1, kabla ya dakika ya 67 Seif Karihe kupachika bao la pili, jitihada, matamanio ya ubingwa yaliwafanya Yanga kusaka bao la kusawazisha na Mudathir Yahya kusawazisha dakika ya 70.

Dakika ya 88 wengi wakiamini mchezo umeisha, Farid Mussa alipachika bao la tatu akiunganisha mpira uliopigwa kona na Mudathir, furaha za shangwe zilikuwa hazina mfano baada ya bao hilo.

Dakika ya 90 Mudathir tena aliandika bao la nne baada ya jitihada zake binafsi za kuwapunguza mabeki wa Dodoma.

Habari Zifananazo

Back to top button