Yanga, GSM wasaini mkataba wa Sh Bil. 11

KLABU ya Yanga na Kampuni ya GSM wamesaini mikataba miwili yenye thamani ya jumla ya Sh Bil 10.9

Akizungumza wakati wa kusaini mikataba hiyo, Dar es Salaam leo, Rais wa Yanga,   Mhandisi Hersi Said, amesema  mkataba huo umegwanyika sehemu mbili.

“Mkataba huo uliogawanyika sehemu mbili utahusisha, mkataba wa kwanza wa uzalishaji na usambazaji wa jezi pamoja na bidhaa mbalimbali za klabu, ambapo kila mwaka GSM Group itailipa Young Africans  Sh  Bilioni 1.5,  ambayo itakua inaongezeka kwa 10% na kufanya jumla ya thamani kuwa  Sh Bilioni 9.15 ndani ya miaka mitano.

“Mkataba wa pili utakua ni wa udhamini, ambapo GSM italipa Sh Milioni 300 kwa mwaka, itakayokuwa ikiongezeka kwa 10% kila mwaka kwa muda wa miaka 5 kuifanya jumla kuwa na Sh Bilioni 1.83 kwa miaka mitano,” alisema Hersi na kuongeza kuwa mkataba huo wa pili ni wa GSM kuweka nembo kwenye jezi.

“Yanga itanufaika na mikataba hii miwili kwa kuvuna takribani Sh Bil. 10.9, jambo ambalo ni neema kubwa kwa Yanga na tunaamini kupitia mikataba hii, Yanga itazidi kuimarika,” alisema Hersi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Biashara, GSM, Allan Chonjo, alisema ameafiki  ufunguzi huo wa ukurasa upya baina ya GSM na Yanga, kwani utakuwa ni chachu ya kudumisha michezo nchini.

Habari Zifananazo

Back to top button