Yanga haitaki dharau ASFC

Mayele

KOCHA Msaidizi wa Yanga,  Cedric Kaze amewataka wachezaji wake kutozidharau timu ambazo wamepangwa nazo kwenye hatua za awali za Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Akizungumza HabariLEO, kocha huyo ameeleza kuwa wachezaji wengi wakubwa wamekuwa hawapendi kucheza mechi hizo na hata wakicheza hawajitoi kama wanapokutana na timu nyingine kwenye ligi.

“Wachezaji watambue haya ni mashindano ya mtoano, ili ufike fainali ni lazima uifunge kila timu unayokutana nayo bila kujali ukubwa wake, hivyo kudharau timu ndogo kunaweza kufifisha malengo tuliyokusudia kuyafikia msimu huu,” amesema Kaze.

Advertisement

Yanga keshokutwa Jumapili watacheza na Rhino Rangers ya Tabora huo ukiwa ni mchezo wa raundi ya tatu wa michuano hiyo ambayo miamba hiyo ndio mabingwa watetezi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *