”Yanga ina wachezaji bora kuliko Mamelodi“

DAR ES SALAAM: KUELEKEA mchezo wa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe amesema hakuna shaka ya aina yoyote wanaenda kushinda mchezo wao dhidi ya Mamelodi Sundowns kwani wana wachezaji bora kuliko timu hiyo.

Akizungumza kwa majigambo katika ofisi za Makao Makuu ya Yanga, Mtaa wa Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam, Kamwe amesema wanaelekea katika mchezo huo utakaopigwa Machi 30, 2024  Uwanja wa Benjamin Mkapa huku wakitambua fika wachambuzi wengi na waandishi hawaipi nafasi Yanga kushinda mchezo huo.

“Nina uhakika wachezaji sita mpaka saba wanaweza kuanza kwenye kikosi cha Mamelodi. Tunaichukulia poa Young Africans SC kwa sababu tu inatokea Tanzania. Lakini hii Klabu ingekuwa ipo DR Congo ingesifiwa sana kuliko inavyosifiwa sasa,” amesema Kamwe.

Advertisement

“Nina uhakika kwa zaidi ya asilimia 100 kuwa tunakwenda kushinda mchezo ujao. Mtu akikwambia Mamelodi ina wachezaji wazuri mwambie hata sisi tuna wachezaji bora kuliko wao,” amesema @alikamwe