Yanga kuondoka leo

Yanga SC inaondoka leo mchana kuelekea nchini Dubai ambapo baada ya mapumziko mafupi kesho wataelekea Tunisia kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya US Monastir utakaopigwa Jumapili hii.

Afisa habari na mawasiliano wa timu hiyo, Ali Kamwe amesema kikosi hicho kinasafiri na wachezaji 25 na benchi la ufundi lenye watu tisa. Kocha wa timu hiyo Nasreddine Nabi ametangulia Tunisia.

“Aboutwalib Mshery ataenda kwa ajili ya matibabu na mwalimu Nabi akiwa ameshatangulia Tunisia kwa ajili ya maandalizi.” Ally Kamwe.

Baada ya mchezo huo Yanga itarejea nchini kujiandaa na mchezo mwingine dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam Februari 19, 2023.

Habari Zifananazo

Back to top button