Yanga kutambulisha mashine mpya leo

RAIS wa Klabu ya Yanga, Hersi Said amesema leo wanatarajia kutambulisha mchezaji mwingine ambaye huko anakotoka alikuwa Mchezaji Bora wa Msimu.

Pia amesema wamejiandaa vizuri kufanya tamasha kubwa la kihistoria Jumamosi wiki hii katika kilele cha Siku ya Mwanachi Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Hersi amesema hayo Julai 19, 2023 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila, wakati wa tukio la kuchangia damu, lililoratibiwa na klabu ya Yanga.

“Jana tulimtambulisha mchezaji atakaevaa jezi namba sita, tumeandika historia ya mchezaji raia wa Afrika Kusini kucheza kwenye ligi yetu na leo usiku tunashusha mchezaji mwingine, ambaye alikuwa mchezaji bora kwenye ligi anayotoka,”ametamba Hersi.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button