Yanga kuwania Kombe Sauzi

AFRIKA KUSINI; Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, imealikwa kushiriki michuano ya Toyota 2024 nchini Afrika Kusini, ambapo itacheza na Kaizer Chiefs kwenye Uwanja wa Toyota mjini Bloemfontein, Afrika KusiniΒ  Julai 28, 2024.

Kurasa rasmi za klabu hiyo zimechapisha picha mbalimbali zikimuonesha Rais wa Yanga, Hersi Said akiwa Afrika Kusini zikiwa na maneno yafuatayo:

“Kama Young Africans Sports Club, tumefurahi sana kupata mwaliko huu wa kushiriki michuano ya Toyota Cup 2024. Mechi hii inaendeleza uhusiano kati ya timu zetu mbili kubwa barani Afrika, ambayo ilianza mwaka jana tulipowaalika Chiefs kushiriki maonyesho yetu, mechi ya kirafiki iitwayo 𝐖𝐒𝐀𝐒 𝐘𝐚 𝐌𝐰𝐚𝐧𝐚𝐧𝐜𝐑𝐒.

Picha zote kwa hisani ya Yanga.

“Tumefurahishwa na mwaliko huu na tunaahidi kutoa mechi ya ushindani ambayo itatusaidia kujiandaa kwa msimu mpya wa 2024/25” imesema taarifa hiyo ikimnukuu Hersi Said.

 

Habari Zifananazo

Back to top button