Yanga mwendo wa ubingwa tu!

ZANZIBAR: Yanga imetetea ubingwa wake wa Kombe la Shirikisho kwa mara ya tatu mfulizo baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 6-5 dhidi ya Azam mchezo uliofanyika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Hii inakuwa mara ya pili mfululizo kwa Yanga kupata ushindi kwa Azam FC kwenye Kombe la Shirikisho, ambapo msimu wa 2022/23 iliibuka na ushindi wa bao 1-0, fainali iliyopigwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga, wakati huo likiitwa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), wakati leo imetwaa Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB.

Timu hizo zilimaliza dakika 90 bila kufungana na ndipo zilipoongezwa dakika 30, lakini pia hazikutoa mshindi, hivyo kwenda katika changamoto ya mikwaju ya penalti.

Penalti za ushindi  Yanga kwenye mchezo huo zilikwamishwa wavuni na Pacome Zouzoua,  Yao Koussi,  Bakari Mwamnyeto. Khalid Aucho, Kennedy Musonda na  Jonas Mkude

Huku waliokosa ni Stephane Aziz Ki ambaye amekosa baada ya kipa wa Azam FC kuupangua sawa na Joseph Guede,  wakati Ibrahim Abdulla ‘Bacca’ penalti yake ilipaa juu ya lango.

Upande  Azam FC waliopata penalti ni  Adolf Mtasigwa, Cheikh,  Kipre Junior,  Edward Manyama na Feisal Salum huku waliokosa ni Yeison Fuentes, Gibli Sillah , Lusajo Mwaikenda na Idd Seleman ‘Nado’.

Yanga walifanya mabadiliko kadhaa kwa kuwatoa Clement Mzize /Joseph Guede Mudathir /Kennedy Musonda, Max Nzengeli/ Jonas Mkude na Joyce Lomalisa/ Bakari Mwamnyeto

Azam FC nao walifanya mabadiliko kadhaa ya kuwapumzisha, Yahya Zayd/ James Akaminko. Abdul  Seleman / Idd Nado, Yannick Bangala   / Edward Manyama na Msindo /  Cheikh Sidibe

Vikosi cha Azam FC,  Mohammed Mustafa,  Lusajo Mwaikenda,  Pascal Msindo,  Yeison Fuentes.  Yannick  Bangala, Adolf Mtasigwa,  Abdul  Hamis,  Yahya Zaydi. Kipre Junior na Feisal Salum ‘Fei Toto ‘.

Yanga: Djigui Diarra, Yao Koussi. Joyce Lomalisa. Ibrahim Bacca. Dickson Job,  Khalid Aucho,  Max Nzengeli, Mudathir Yahya,  Clement Mzize. Stephen Aziz Ki na Pacome Zouzoua.

Habari Zifananazo

Back to top button