Yanga, Nyasa BB hakuna mnyonge

MCHEZO wa kirafiki wa kusherehesha Siku ya Uhuru nchini Malawi kati ya Yanga SC na Nyasa Big Bullet umemalizika kwa sare ya 0-0 uwanja wa Bingu.

Mchezo huo umeshuhudiwa pia na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera.

Awali kabla ya mchezo huo viongozi hao walikutana Ikulu ya Lilongwe, Ofisi za Bunge la Malawi na baadaye uwanjani kushuhudia mchezo huo.

Advertisement

Kikosi cha Yanga katika mchezo huo, Metacha Mnata, Maulid Tamila, Mohammed Omar, Shaibu Mtita, Joyce Lomalisa, Khamis Nangukha, Crispin Ngushi, Denis Nkane, Sharifu Kimbowa, Clement Mzize na Moses Aliao.

Kikosi cha Nyasa BB, Chimbamba, Kaonga, Mpokera, Banda, Foydi, Kabichi, Phiri, Mgwira, Singo, Pasua na Kondowe.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *