‘Yanga Stadium’ inakuja tulia uone

MDHAMINI na mfadhili wa klabu ya Yanga, Gharib Said Mohammed (GSM) ameridhia kujenga uwanja katika eneo la makao makuu ya klabu hiyo Jangwani Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa leo Februari 11, 2024 na Rais wa Yanga,  Hersi Said imeeleza kuwa  uongozi wa Yanga upo tayari kumpa ushirikiano GSM katika mchakato wote wa ujenzi wa uwanja huo.

Aidha taarifa hiyo imefafanua kuwa kuridhia kwa GSM juu ya suala hilo kumetokana na mazungumzo yaliyoanza muda mrefu uliopita.

Yanga inaadhimisha miaka 89 ya kuanzishwa kwake ambapo Hersi amewapongeza viongozi wote waliomtangulia katika kufanikisha mengi klabuni hapo.

Habari Zifananazo

Back to top button