“Yanga tunataka kuongoza kundi”

DAR ES SALAAM: Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema hawaendi nchini Misri kutalii bali wanafuata ushindi katika mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Ijumaa hii.

Kamwe amesema wanazifahamu faida za kumaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi hivyo dhamira yao ni kunufaika na matunda hayo

“Kuna watu wanasema tunakwenda kutembelea Pyramids na kununua kanzu, nafikiri mmeona namna ambavyo tumejiandaa kwenda kwenye mchezo huo, maandalizi haya sio kwa ajili ya kwenda kutalii ni kwa ajili ya kwenda kupambana hata kama tumeshafuzu” amesema Kamwe na kuongeza

Advertisement

“Tunataka kuongoza kundi, ili tupate faida ya kuanza mchezo wetu wa robo fainali ugenini, tunataka kucheza na walioshika nafasi ya pili.”

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka leo hii kwenda nchini Misri kwa ajili ya mchezo huo.

 

/* */