Yanga ubingwa huu hapa
BAADA ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Big Stars, Yanga imejiweka mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ikiwa na tofauti ya pointi 7 dhidi ya Simba SC, huku ikiwa imebaki michezo mitatu ligi kumalizika.
Yanga sasa inahitaji ushindi wa mchezo mmoja ili kutangazwa mabingwa wapya wa ligi hiyo msimu wa 2022/2023.
Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Liti, kiungo Aziz Ki alikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza dakika ya 15, baada ya kupiga shuti lililomshinda mlinda mlango wa Singida, Benedict Haule.
Dakika ya 21 mshambuliaji Clement Mzize alipigilia msumari wa pili na kukamilisha ushindi huo na Yanga kutwaa pointi tatu.