Yanga utamu kolea kimataifa

NDOTO za Yanga kutinga Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, zimetimia leo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya US Monastir ya Tunisia.
Matokeo hayo yameifanya Yanga kufikisha pointi 10 sawa na Monastir, lakini Yanga wanakaa kileleni mwa Kundi D kutokana na wastani mzuri wa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Mabao ya Yanga katika mchezo huo yamefungwa na Kennedy Musonda dakika ya 33 na Fiston Mayele dakika ya 59.