Medeama Vs Yanga mechi iliyobeba hatma

KUMASI, Ghana: Mabingwa wa kandanda nchini, Yanga leo wanatupa karata muhimu mno katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika watakapokuwa wageni wa Medeama ya Ghana katika mchezo wao wa tatu wa makundi ya michuano hiyo.

Huu ni mchezo uliobeba dira ya wababe hao wa mitaa ya  Twiga na Jangwani kwani kama watashinda mchezo huo basi watatengeneza ramani nzuri ya kuisaka robo fainali ya mitanange hiyo.

Yanga wanaingia katika mchezo huo wakiburuza mkia katika kundi D wakiwa na alama moja pekee wakati Medeama yeye anashika nafasi ya tatu wakiwa na alama tatu timu ya CR Belouizdad inashika nafasi ya pili kwenye kundi hilo ikiwa na alama tatu nyuma ya vinara Al Ahly yenye alama nne.

Advertisement

 

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *