Yanga waachana na Moloko

YANGA imeachana na winga Jesus Moloko baada ya makubaliano rasmi ya pande zote mbili.

Yanga imetoa taarifa hiyo leo kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Moloko amepewa barua leo Januari 15 asubuhi ambapo nafasi yake tayari amesajiliwa Mghana Augustine Okrah.

“Young Africans SC tumefikia makubaliano ya pande zote mbili kusitisha mkataba na mchezaji Jesus Ducapel Moloko.” Imeeleza taarifa ya Yanga.

 

Habari Zifananazo

Back to top button