Yanga waifukuzia ‘Unbeaten’ ya 50

UMEBAKI mchezo mmoja Yanga wafiishe michezo 50 bila kufungwa, baada ya leo kufikisha 49 kwa kumfunga Mbeya City mabao 2-0 Uwanja wa Mkapa.

Fiston Mayele ameendelea kuwa tishio kwa timu pinzani, baada ya kufunga mabao yote mawili na kufikisha jumla ya mabao 10 katika msimamo wa wafungaji wa Ligi Kuu.

Advertisement

Matokeo hayo yanaendelea kuwaimarisha Yanga katika nafasi ya kwanza, ikiwa na pointi 32, na michezo 12. Nyuma ya Azam FC wenye 29, Simba SC, 28 ikiwa nafasi ya tatu, na michezo 13.