Yanga wajichimbia kileleni

SOKOINE, Mbeya: MABAO 2-1 ya Yanga SC dhidi ya wenyeji Tanzania Prisons SC yamewafanya wababe hao wa mitaa ya Twiga na Jangwani kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na alama 40 katika mechi 15.

Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, umeshuhudia kipindi cha kwanza Yanga wakimaliza dakika 45′ wakiwa mbele kwa mabao mawili, mfungaji ni Clement Mzize dakika 8′ na Pacome Zouzoua dakika 45+3′.

Kipindi cha pili, dakika 64′ Jeremiah Juma akaiandikia Prisons bao la kufutia machozi kwa njia ya adhabu ndogo iliyochongwa nje kidogo ya eneo la 18 la mabingwa watetezi.

Prisons wanasalia nafasi ya 9, alama 17 katika michezo 15.

Pasi na shaka keki ya Yanga SC kusherehekea kumbukizi ya miaka 89 ya kuanzishwa kwake ipo bukheri wa salama.

Habari Zifananazo

Back to top button