Yanga wakabidhiwa Sh Mil 5 za Samia

Yanga wakabidhiwa Sh Mil 5 za Samia

MKURUGENZI wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa leo Februari 28, 2023 ameikabidhi Yanga Sh milioni 5, ikiwa ni ahadi ya Rais Samia Suluhu ya kutoa Sh milioni 5 kwa bao litakalofungwa na timu za Simba na Yanga katika michuano ya kimataifa.

Yanga imekabidhiwa fedha hizo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Real Bamako ya Mali katika mchezo wa raundi ya tatu wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Advertisement
Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *