Yanga wimbo ushindi Singida kesho

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema Singida Big Stars haiwezi kuwa kikwazo cha wao kushindwa kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu msimu huu.

Akizungumza na HabariLEO, kocha huyo ameeleza kuwa wanajua benchi la ufundi pamoja na kila mchezaji wanatambua umuhimu wa ushindi,  hivyo kuelekea mchezo huo utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa Liti Singida wamejipanga vizuri kuhakikisha wanaondoka na pointi zote tatu.

“Ni kweli Singida msimu huu imeongeza ushindani lakini haiwezi kutuzuia Yanga kushindwa kutimiza malengo yetu, najua mchezo utakuwa mgumu lakini baada ya dakika 90 pointi tatu zitabaki Yanga,” amesema Kaze.

Yanga kesho watakuwa ugenini kukabiliana na wenyeji Singida Big Stars katika mchezo wa raundi ya 27 wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button