MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe amesema serikali ya Malawi imeialika timu hiyo kutoa burudani katika maadhimisho ya miaka 59 ya uhuru wa taifa hilo.
Katika sherehe hiyo itakayofanyika Julai 6 ,2023 Yanga watacheza na Nyasa Big Bullets FC.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 3, Kamwe amesema licha ya kutokuwa na ratiba hiyo ila watalazimika kuhudhuria sherehe hiyo.
“Kwa heshima ambayo serikali ya Malawi imetupatia Young Africans, kuona kwamba tunatosha kwenda kutoa burudani kwa Wamalawi wakiwa wanaadhimisha sherehe zao za uhuru, uongozi wa Young Africans ukapiga simu kwa wachezaji kuwaambia kwamba tunatakiwa kwenda Malawi,” amesema Kamwe.
Comments are closed.