Yanga yaifuata Belouizdad

DAR ES SALAAM: Msafara wa klabu ya Yanga umeondoka nchini, kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya, CR Belouizdad ya Algeria utakaopigwa Novemba 24, 2023.
Kikosi hicho kimeondoka nchini bila ya baadhi ya nyota wao ambao wapo kwenye majukumu ya timu za taifa, hata hivyo taarifa kutoka ndani ya timu hiyo zimeeleza kuwa wachezaji hao watajiunga moja kwa moja na kambi ya timu hiyo nchini Algeria kuanzia kesho.

Habari Zifananazo

Back to top button