Yanga yakamata nafasi ya pili kundi D CAF

USHINDI wa mabao 3-0 dhidi ya Medeama, umeisogeza Yanga nafasi ya pili katika msimamo wa kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika, huku wakisubiri matokeo ya Al-Ahly dhidi ya CR Belouizdad.

Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Mkapa Dar es Salaam, mabao ya Yanga yalifungwa na Pacome Zouzoua dakika ya 33, Bakari Mwamnyeto dakika ya 61 na Mudathir Yahya dakika ya 70.

Yanga sasa imefufua matumaini ya kucheza robo fainali baada ya kukusanya jumla ya pointi tano, akiwa sawa na Al-Ahly wenye idadi hiyo ya pointi.

Baada ya mchezo huo, Yanga itamaliza nyumbani kwa mchezo dhidi ya CR Belouizdad.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button