Klabu ya Yanga imetozwa faini ya Sh milioni 2 na Bodi ya Ligi Kuu kwa makosa mawili.
Katika mchezo dhidi ya Ihefu uliochezwa wiki mbili zilizopita, baadhi ya mashabiki wa Yanga walirusha chupa za maji kiwanjani baada ya timu ya Ihefu kufunga bao la pili, hilo kosa la kwanza.
Kosa la pili, maofisa wa benchi la ufundi wa Yanga kuonekana wakipinga maamuzi na kumzonga mwamuzi wa akiba.
Kila kosa limetozwa faini ya Sh milioni 1.