Yanga yalimwa faini ya Shilingi milioni 5

Chama, Aziz Kii wafungiwa

 

KLABU ya Yanga imepigwa faini ya shilingi milioni 5 kwa kosa la kuingia chumba cha kubadilishia nguo kupitia mlango usio rasmi kuelekea mchezo dhidi ya Simba SC uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa Oktoba 23, mwaka huu.

Barua iliyotolewa na Shirikisho la soka nchini (TFF) imeeleza kuwa adhabu hiyo imezingatia kanuni ya 17:(21-60) ya Ligi Kuu kuhusu michezo.


Aidha, wachezaji wa timu hizo, Aziz Ki na Clatous Chama wamefungiwa michezo mitatu na kutozwa faíni ya Shilingi 500,000 kwa kosa la kukwepa kusalimíana na wachezaji wa timu pinzani kabla ya kuanza kwa mchezo wa dabi ya Kariakoo.

Mwamuzi Florentina Zabron aliyechezesha mchezo wa Geita Gold na Yanga atafikishwa kwenye kamati ya waamuzi kwa kosa la kushindwa kitafsiri sheria 17 za soka na kupelekea kutoa penati

Habari Zifananazo

Back to top button