Yanga yamnyima raha Pluijm

KOCHA Mkuu wa Singida Big Stars, Hans Pluijm amekiri kuwa ubora wa kikosi cha Yanga unamnyima usingizi kuelekea mechi mbili ambazo wanatarajia kucheza hivi karibuni.

Akizungumza na HabariLEO, kocha huyo amesema kuwa kiwango na matokeo inayoyapata timu hiyo kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, inaonesha namna ilivyo bora hivi sasa.

“Hakuna kocha ambaye anapenda kukutana na Yanga katika kipindi hiki kutokana na ubora wao, hii ni timu ambayo imeimarika sana na wamekuwa wakipata ushindi sehemu yoyote, kitu ambacho kinatupasa kuwa makini,” amesema Pluijm.

Singida Big Stars itacheza na Yanga mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Tanzania Bara Mei 4 na siku tatu baadaye itarudi tena uwanjani kucheza na timu hiyo kwenye mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam  (ASFC), mechi zote zikitarajia kupigwa Uwanja wa Liti mkoani Singida.

Habari Zifananazo

Back to top button