Yanga yamteua Nkoma kuifundisha Princess

Uongozi wa klabu ya Yanga umemtangaza Sebastian Nkoma kuwa kocha wa timu yao ya Wanawake ya Yanga Princess akilamba mkataba wa mwaka mmoja.

Nkoma aliwahi kuifundisha Simba Queens na kufanikiwa kubeba kombe la Ligi Kuu ya Wanawake akiwa na kikosi hicho.

Amewahi kuzifundisha timu mbalimbali za Wanaume kwenye Ligi Kuu, ikiwemo Majimaji ya Songea, Moro United na Rhino Rangers.

Aidha aliwahi pia kuteuliwa na TFF kuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu ya Taifa ya vijana ya Serengeti Boys iliyofuzu AFCON mwaka 2017.

Baadaye kocha Nkoma alipewa timu ya taifa ya Wanawake, Twiga Stars kabla ya kuifundisha timu ya Wanawake ya Simba Queens.

Habari Zifananazo

Back to top button