Yanga yamuahidi makubwa Rais Samia

KLABU ya Yanga imemuahidi Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wataendelea kupambana katika michuano ya kimataifa na ikiwezekana kufika hadi fainali kwa lengo la kuitangaza Tanzania.

Hayo yamesemwa leo na Meneja wa Habari wa timu hiyo, Ally Kamwe wakati akikabidhiwa kitita cha Sh Milioni 10 zilizotokana na ushindi wa mabao 2-0 ugenini katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya robo fainali waKombe la Shirikisho dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

“Tuna mshukuru Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ahadi ake kwa vitendo tumepokea pesa hizi na kiukweli zimetupa hamasa kubwa hadi kufika hapa sisi Yanga tunamuahidi kuipeperusha bendera ya nchi hii kwa kufika mbali ikiwezekana kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho,” amesema Kamwe.

Yanga Jumapili hii itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kurudiana na Rivers United na inahitaji sare au ushindi wowote ili kuandika historia ya kutinga Nusu Fainali ya michuano hiyo kwa timu za Tanzania.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button