Yanga yapewa tano bungeni

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ameimwagia sifa timu ya Yanga kwa uwakilishi mzuri kwenye michuano ya kimataifa na kuitaka kuendelea kujiimarisha, ili kufanikiwa zaidi.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2023/2024 , Aweso ameitakia kila la heri Yanga kwenye mchezo wake wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika leo jioni dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika kusini.

“Naomba nitoe pongezi za dhati kwa Dar Young Africans kwa kuendelea kuupiga mwingi ndani na nje ya nchi katika kuhakikisha kwamba inaliwakilisha vyema taifa letu.

” Hapa niseme asiyekubali kushindwa sio mshindani, leo Yanga wanaenda kuliwakilisha taifa letu, ukizaa mtoto anafanya vyema jukumu lako ni kumuombea dua tunawaombea dua sana Dar Young Africans hii leo,” amesema.

Aidha Waziri Aweso ameipongeza timu ya Simba kwa hatua iliyofikia kwenye ligi ya mabingwa msimu huu na kuitaka kujipanga vyema kwa ajili ya msimu ujao.

Habari Zifananazo

Back to top button