Yanga yapigwa pini kusajili

Rais wa Yanga, Hersi Said

DAR ES SALAAM: KLABU ya @yangasc imekutana na rungu jingine la kufungiwa kusajili wachezaji wapya kwa msimu wa 2024/25 kutokana na kukiuka kanuni za usajili za FIFA.

Imeelezwa kuwa mchezaji anayeidai Yanga ni Hafiz Konkonim ambaye alivunjiwa mkataba wake kwenye dirisha dogo lililopita na nafasi yake kuchukuliwa na Joseph Guede.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), iliyotoka Juni 18, imezitaka klabu zote zinazodaiwa  na wachezaji wao kuwalipa haraka kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Advertisement