Yanga yapotezwa adhabu ya Aucho

DAR ES SALAAM: Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeeleza kuwa kiungo wa Yanga, Khalid Aucho ataendelea kuitumikia adhabu yake kama ilivyoelezwa hapo awali.
Taarifa iliyotolewa Desemba 15, 2023 na kamati hiyo imeeleza kuwa kamati imejadili maombi ya marejeo ya klabu ya Yanga kuhusu adhabu ya kufungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya Sh laki tano (500, 000) iliyotolewa kwa Aucho.
Hata hivyo baada ya kupitia hoja hizo na kujirudhisha tena kamati imeona maamuzi ya hapo awali yalikuwa sahihi hivyo mchezaji huyo ataendelea kutumikia adhabu hiyo.

Habari Zifananazo

11 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button