Yanga watamba sherehe za miaka 89

ILALA, Dar es Salaam: YANGA SC imeweka wazi ratiba nzima ya tukio kubwa la kihistoria kwa klabu hiyo katika kusherehekea miaka 89 tangu kuanzishwa kwake Februari 1935.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maskani ya klabu hiyo mitaa wa Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam, Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ally Kamwe amesema tukio hilo kubwa litakalofanyika jijini Mbeya litatanguliwa na uzinduzi wa nyimbo mbili kubwa zitakazoleta ‘amsha amsha’ siku hiyo.

“Tunakwenda kuzindua nyimbo mbili kubwa kwa lengo la kusheherekea kilele cha ‘anniversary’ ya mabingwa wa kihistoria. Yaani kuelekea kwenye hiki kilele ni jiwe juu ya jiwe. Hakupoi, kila mwanachama anapaswa kuweka kambi Mbeya.” Amesisitiza meneja huyo.

Advertisement

Yanga ilianzishwa mwaka 1935, mwaka huu inatimiza miaka 89, ndio bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikitwaa mara nyingi 29.

Yanga pia wanakishikilia rekodi ya michezo mingi zaidi bila kufungwa ‘unbeaten’ ikicheza michezo 49 bila kufungwa msimu wa 2022/23. Mafanikio makubwa wa klabu hiyo kimataifa ni kucheza hatua ya fainali katika Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC 2023).

/* */