Yanga yatemana na Moloko

MTANDAO: YANGA SC imetangaza kuachana na kiungo wa pembeni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (DRC), Jesus Moloko kwa makubaliano ya pande mbili
Yanga SC wametangaza taarifa hiyo kupitia mitandao yao ya kijamii hii leo.
“Tumefikia makubaliano ya pande zote mbili kusitisha mkataba na mchezaji Jesus Ducapel Moloko.” Imeeleza taarifa hiyo.
Moloko alijiunga na Yanga katika dirisha kubwa la usajili, Agosti 2021 akitokea AS Vita ya DRC.

Habari Zifananazo

Back to top button