Yanga yatoa pole kifo cha Madega

UONGOZI wa Yanga umetoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Iman Madega aliyefariki dunia leo wilayani Chalinze mkoani Pwani.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo leo Februari 10, 2024 imeeleza kuwa maziko ya Madega yatafanyika kesho saa 10:00 Alasiri wilayani humo.

“Hili ni pigo kubwa kwa klabu yetu ya Young Africans, na familia ya michezo nchini, sisi Young Africas, tutamkumbuka mzee Madega kwa mapenzi yake makubwa, aliyokuwa nayo kwa klabu yetu”. Imeeleza taarifa hiyo.

Advertisement

Madega aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Yanga kuanzia mwaka 2006 hadi 2010.

Kiongozi huyo amefariki akiwa Chalinze, Pwani.