Yonas: pimeni afya, fanyeni kazi kwa upendo
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt.
Jim Yonas amewataka watumishi wa ofisi hiyo kuacha tabia bwete, kufanya mazoezi na kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara.
Dk Yonas ameyasema hayo akifungua kikao chake na watumishi wa ofisi hiyo na kuwataka kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuyafikia malengo ya Serikali.
“Tumepata fursa ya kukumbushwa kupima afya zetu, hii ni changamoto inayotukabili, hivyo ni muhimu kuzingatia ushauri wa afya na masharti ya namna ya kuboresha masuala yanayohusu afya zetu.” Amesema Yonas na kuongeza
“Falsafa yangu ni kuona watu ninaowaongoza wanafanya kazi kwa upendo na kushirikiana, napenda kufanya kazi na watu wanaoheshimiana na wenye amani siamini kama mtu anaweza akafikiri vizuri iwapo hana amani ndani.”Amesema