Yusuf Manji kuzikwa leo Florida

MAREKANI – ALIYEKUWA mwenyekiti na mfadhili wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji atazikwa leo Florida nchini Marekani, familia yake imesema.

Mfanyabiashara huyo aliefariki dunia Jumamosi Juni 29, 2024 saa 6 usiku akiwa hospitalini alipokuwa anapatiwa matibabu.

Taarifa za kifo cha Manji zimethibitishwa na vyombo mbalimbali huku vingine vikimnukuu mtoto wake, Mehbub Manji.

Advertisement