Zahanati Bugogo sasa yaanza kazi

ZAHANATI ya Kijiji cha Bugogo, Kata ya Mwamala, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga iliyodaiwa kufungwa baada ya mganga aliyekuwepo kufariki, sasa imefunguliwa na kuletwa mwingine ambaye ameanza kutoa huduma.

Zahanati hiyo ilikuwa na watumishi wawili , ambapo muuguzi pekee ndiye aliyebaki na kuelemewa na utoaji wa huduma zote ikiwemo uzalishaji wa wajawazito na huduma za kliniki kwa watoto takribani zaidi ya miezi sita.

Wakizungumza na HABARILEO leo baadhi ya wananchi wa kijiji hicho , akiwemo Diana Tungu alisema zahanati hiyo imefunguliwa na kuanza kutoa huduma na mganga ameanza kufanya kazi.

Advertisement

“Tulikuwa tunakwenda Kituo cha Afya Samuye umbali wa kilomita 15 kupata huduma, hata kijiji jirani cha Mwamala ni mbali tumeteseka hasa wajawazito na watoto,”alisema Tungu.

Muuguzi Lenny Kinkoro alisema alipata changamoto kubwa kuwa peke yake kwenye utoaji wa huduma kwa wagonjwa takribani 20 kwa siku na wajawazito wanaojifungua takribani 12 kwa siku na huduma za kliniki.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *