Zahera kocha mpya Coastal Union
TIMU ya Coastal Union ya Tanga imemteua Mwinyi Zahera kuwa kocha mkuu.
Zahera raia wa Congo DR amesaini mkataba wa mwaka mmoja, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na timu hiyo.
Kocha huyo amewahi kuzifundisha timu za Yanga na Polisi Tanzania.
Uteuzi wa Zahera unazima tetesi za kwamba huenda kocha msaidizi wa Simba SC, Juma Mgunda angereje kwenye timu hiyo.