Zaidi ya magari 2000 hupakuliwa bandari ya Dar kila siku

MAMLAKA ya Bandari nchini (TPA) imesema inapokea zaidi ya magari 2,000 kila siku kupitia Bandari ya Dar es Salaam ambapo asilimia 60 ya magari hayo huenda nchi jirani.

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho amewaambia wanahabari mjini Bagamoyo wakati wa kikao kazi kuwa Idadi hiyo inatokana na maboresho katika Bandari hiyo ikiwa ni pamoja na maboresho katika eneo lenye ukubwa mita za mraba 76,000.

Mrisho amesema eneo hilo kwa sasa linauwezo wa kubeba magari zaidi ya 6,000 na limefungwa na miundombinu ya kisasa kuwezesha ulinzi na usalama.

Mkurugenzi wa Huduma za Usalama katika Mamlaka ya Bandari nchini amesema kuna zaidi ya kamera za ulinzi (CCTV) 450 ambazo zimefungwa katika bandari ya Dar es Salaam ili kuimarisha usimamizi wa bandari hiyo.

Mpanda amesema, Mamlaka pia imefunga midaki (Scanners) katika bandari hiyo ili kubaini mizigo ambayo imepakiwa kwenye makasha (containers). Akizungumza na wanahabari katika kikao kazi kinachoendelea Bagamoyo mkoani Pwani, Mpanda amesema Mamlaka pia inaendelea na mpango wa kuunganisha Bandari zote 86 katika mfumo wa kisasa utakao wezesha utambuzi wa shughuli zote katika bandari.

“Tumeweka mifumo hii ya kiteknolojia lakini pia kuna askari na doria ambazo zinafanyika ili kuhakikisha usalama na kudhibiti uhalifu bandarini,” amesema Mpanda.

Habari Zifananazo

Back to top button