Zaidi ya Sh bilioni 48 kutumika ukarabati wa Meli

MWANZA: Serikali kupitia Kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), imesaini mikataba mitatu yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 48 kwaajili ya ukarabati wa Meli kongwe ya abiria ya Mv. Liemba iliyopo ziwa Tanganyika,Meli ya mafuta Mt.Nyangumi na Meli ya kutolea msaada(uokozi) ikiwemo kuvuta meli nyingine Mt.Ukerewe zote zipo ndani ya Ziwa Victoria.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi ,David Kihenzile pia kulishuhudiwa tukio la uzinduzi wa Meli ya mizigo ya Mv.Umoja”KAZI IENDELEE “baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa uliogharimu kiasi cha Sh bilioni 21 ambapo itakuwa na uwezo wa kubeba tani 1,200 za mizigo.
1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *