Zaidi ya watu 1,100 wauawa Gaza

ZAIDI ya watu 1,100 wakiwemo Wapalestina 436 wameuawa katika mapigano yanayoendelea kati ya kundi la Hamas na jeshi la Israeli.

Israel imekuwa ikirusha makombora yake kwa miaka 15 iliyopita huko Palestina na kuuwa baadhi ya watoto, wanawake na wazee.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa zaidi ya watu 123,000 hawana makazi Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa mapigano hayo.

Advertisement

“Hii imetokana na hofu, kutokuwa na ulinzi na uharibifu wa makazi ya watu.” Imeeleza ripoti Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *