Wagonjwa 480 watolewa mawe njia mawimbi mtetemo

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imehudumia zaidi ya wagonjwa 480 waliokuwa na changamoto ya mawe kwenye figo kwa kutumia mashine maalumu ya kuvunja mawe kwenye figo kwa kutumia mawimbi mtetemo ((Extracorporeal Shock Wave Lithotripsy-ESWL)

Huduma hiyo ambayo ilianza Juni, 2020  inatolewa katika kliniki ya magonjwa ya mfumo wa mkojo Muhimbili- Mloganzila.

Hayo yamesemwa na daktari bingwa wa upasuaji mfumo wa mkojo, Dk Hamis Isaka alipokuwa akielezea mafanikio ya huduma hiyo ambayo kwa hospitali za umma hapa nchini inatolewa na MNH-Mloganzila pekee.

Advertisement

Dk Isaka amesema kupitia matibabu hayo mawe kwenye figo yanasagwa kwa njia ya mawimbi mtetemo na kuwa chembe ndogo ndogo mithili ya mchanga ambao zinatoka kwa njia ya haja ndogo.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *